MSLAC YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA 61 YA SABASABA: SAUTI YA HAKI KWA JAMII YOTE

Katika Maonesho ya 61 ya Kimataifa ya Biashara ya SabaSaba, yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam – Kampeni ya Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) imeweka historia kwa kujenga kambi rasmi ya utoaji elimu na msaada wa kisheria kwa wananchi , ikiwa ni hatua madhubuti ya kuhakikisha haki inawafikia Watanzania wote, hasa wale wasio na uwezo wa kulipia huduma za kisheria. Mpango huu unatekelezwa kwa weledi chini ya Wizara ya Katiba na Sheria , kwa kushirikiana na watoa huduma mbalimbali wa msaada wa kisheria ikiwemo Taasisi ya Huduma ya Msaada wa Kisheria (LHRC), Tanganyika Law Society (TLS) , taasisi zisizo za kiserikali, vyombo vya sheria, na mawakili wa kujitolea. Lengo Kuu la MSLAC: Kampeni hii inalenga: Kufikisha elimu ya kisheria kwa wananchi kwa lugha rahisi na inayoeleweka, Kutoa msaada wa kisheria katika migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi, ajira, ukatili wa kijinsia, na masuala ya jinai, Kuhamasisha jamii kuhusu hak...