VIONGOZI SONGEA NA MADABA KUPATIWA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO SEKTA YA SHERIA
Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa semina itakayotoa Elimu ya utatuzi wa Migogoro ya sekta ya Sheria kwa viongozi wa kada ya chini wa Manispaa ya Songea Mjini na wa Wilaya ya Madaba. Akizungumza na Timu ya utoaji wa Elimu hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa ili kumaliza migogoro mbalimbali ya kisheria inayoibuka na ile iliyoibuliwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni vyema kuwapatia elimu viongozi hao ili wakabiliane nayo kuanzia ngazi za chini. Aidha Mhe. Dkt Ndumbaro amesema mbali ya utatuzi wa Migogoro pia viongozi hao wapatiwe elimu ya uraia na Utawala bora, Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Elimu kuhusu Uchaguzi Mkuu.







Tunampongeza na kumshukuru Rais wetu wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa na muongozo mzuri katika kipindi hiki Cha uchanguzi ambapo kila mwananchi ana Haki ya kulindwa wakati wa uchaguzi,haki ya kushiriki kampeni za uchaguzi,haki ya kutoa malalamiko,haki ya kupiga kura na haki ya kugombea uongozi.
ReplyDeleteKampeni hii imesaidia sana kupunguza migogoro isiyo ya lazima
ReplyDeleteKila Mwananchi Anahaki ya kuchagua kiongozi anaye mtaka Hivyo kila Mtanzania Ana Haki ya kulindwa pindi anapo fanya Uchaguzi wa Kiongozi amtakaye anaye ona anamfaa
ReplyDelete