Posts

Showing posts from December, 2023

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kurejesha amani katika familia

Image
U tekulizaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia umekuwa na mchango mkubwa katika kurejesha amani na utulivu katika familia na jamii kadhaa zilizokuwa zikikabiliwa na migogoro nchini kote. Kampeni hiyo inatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LSF). Kampeni hii inatekelezwa kama sehemu ya mipango ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuunganisha nchi na kuleta maendeleo katika ngazi zote. Lazima tuhakikishe mizozo yote katika ngazi ya familia na jamii inakwisha. Migogoro mingi ambayo imepatiwa ufumbuzi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni ya:-  Ardhi,  Umiliki wa mali,  Mirathi na  Ukatili wa Kijinsia (GBV). Utawala wa sheria na haki za binadamu,  Kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa utoaji haki na kuboresha. mifumo, sera na sheria ili kuimarisha upatikanaji wa haki nchini. Utekelezaji wa kampeni hii unakwenda sambamba na kuwapatia wananachi huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa wanawake, watoto na makund
Image
   MSAADA WA KISHERIA BAADA YA MAAFA YA KITAIFA KWA WAHANGA Sheria inatoa mwongozo wa jinsi serikali inavyopaswa kushughulikia na kurejesha hali ya kawaida baada ya maafa kutokea. Masuala ya maafa na utawala wa dharura yanaweza kushughulikiwa katika vipengele kadhaa vya Katiba na sheria nyingine nchini. #Katibayawatu #Katibanimaridhiano Baadhi ya vipengele vinavyohusiana na maafa katika Katiba ya Tanzania: Ibara ya 10: Inaelezea kanuni za msingi za utawala wa sheria na inaweza kutoa muktadha wa jinsi serikali inavyopaswa kushughulikia masuala ya dharura na maafa kwa kuzingatia kanuni za haki na sheria. Ibara ya 11(1): Inaelezea kwamba mamlaka ya nchi inatokana na wananchi, na mamlaka hiyo inatekelezwa kwa mujibu wa Katiba. Hii inaweza kutoa msingi wa kisheria kwa hatua zinazochukuliwa wakati wa maafa. Ibara ya 17(1): Inaelezea haki ya kuishi na haki nyingine za msingi za binadamu. Hii inaweza kuwa na uhusiano na masuala ya maafa na jinsi serikali inavyopaswa kulinda haki hizi wakati w
Image
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campaign   Kampeni hii inafanyika kwa miaka mitatu kuanzia mwezi Machi, 2023 hadi mwezi Februari, 2026 katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.  Kampeni imejikita katika kutoa elimu ya kisheria kwa wananchi hususan katika masuala ya ukatili wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala, na masuala yahusuyo haki za binadamu kwa ujumla. Utekelezaji wa kampeni unafanyika kwa kushirikiana na Wizara na Taasisi za Serikali, Asasi za Kiraia, Wanazuoni na Wadau wa Maendeleo.   Lengo kuu la Kampeni ni ni kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini. Katika kufikia lengo hilo, kampeni inaongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususan haki za wanawake na watoto; Inatoa  huduma ya  ushauri  wa kisheria na unasihi kwa waathirika na manusura wa ukatili wa kijinsia; kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu  elimu ya sheria,  masual