Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kurejesha amani katika familia
U tekulizaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia umekuwa na mchango mkubwa katika kurejesha amani na utulivu katika familia na jamii kadhaa zilizokuwa zikikabiliwa na migogoro nchini kote. Kampeni hiyo inatekelezwa kwa pamoja kati ya serikali na Kituo cha Msaada wa Kisheria (LSF). Kampeni hii inatekelezwa kama sehemu ya mipango ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuunganisha nchi na kuleta maendeleo katika ngazi zote. Lazima tuhakikishe mizozo yote katika ngazi ya familia na jamii inakwisha. Migogoro mingi ambayo imepatiwa ufumbuzi kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni ya:- Ardhi, Umiliki wa mali, Mirathi na Ukatili wa Kijinsia (GBV). Utawala wa sheria na haki za binadamu, Kuwajengea uwezo wadau wa mnyororo wa utoaji haki na kuboresha. mifumo, sera na sheria ili kuimarisha upatikanaji wa haki nchini. Utekelezaji wa kampeni hii unakwenda sambamba na kuwapatia wananachi huduma ya wasaidizi wa kisheria kwa wa...