
MUHADHARA WA WAZI WA KITAALUMA KUTOKA KWA WAKUFUNZI WA OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA MKUU NCHINI URUSI Faida ya muhadhara huu ni; Kuongeza uelewa kwa umma Hii ni kutokana na uwepo wa mada zinazohusiana na sheria na mfumo wa haki kwakuwa ni ngumu kwa watu wengi kuelewa hivyo itasaidia watu wengi kujifunza na kuelewa zaidi. Kuimarisha imani katika mfumo wa haki Hii ni kutokana na kutolewa kwa ufafanuzi wa wazi na wenye msingi wa kisheria hivyo kusaidia kujenga imani ya umma katika mfumo wa haki inayopatikana kwa kuzingatia na kufuata sheria nchini Urusi. Kupambana na ufisadi na unyanyasaji wa mamlaka Kupitia muhadhara huu, inaweza kuwa jukwaa la kufichua mifano ya ufisadi au unyanyasaji wa mamlaka ndani ya mfumo wa haki ya Urusi na itapelekea kuhamasisha mabadiliko na kuboresh uwajibikaji. Kongezwa kwa upana wa uelewa kwa vyombo vingine vya haki na sheria Hii ni fursa pia kwa wataalamu wengine wa sheria na haki kama vile wanasheria, polisi na wachunguzi ku...