MUHADHARA WA WAZI WA KITAALUMA KUTOKA KWA WAKUFUNZI WA OFISI YA MWENDESHA MASHTAKA MKUU NCHINI URUSI
Faida ya muhadhara huu ni;
Kuongeza uelewa kwa umma
Hii ni kutokana na uwepo wa mada zinazohusiana na sheria na mfumo wa haki kwakuwa ni ngumu kwa watu wengi kuelewa hivyo itasaidia watu wengi kujifunza na kuelewa zaidi.
Kuimarisha imani katika mfumo wa haki
Hii ni kutokana na kutolewa kwa ufafanuzi wa wazi na wenye msingi wa kisheria hivyo kusaidia kujenga imani ya umma katika mfumo wa haki inayopatikana kwa kuzingatia na kufuata sheria nchini Urusi.
Kupambana na ufisadi na unyanyasaji wa mamlaka
Kupitia muhadhara huu, inaweza kuwa jukwaa la kufichua mifano ya ufisadi au unyanyasaji wa mamlaka ndani ya mfumo wa haki ya Urusi na itapelekea kuhamasisha mabadiliko na kuboresh uwajibikaji.
Kongezwa kwa upana wa uelewa kwa vyombo vingine vya haki na sheria
Hii ni fursa pia kwa wataalamu wengine wa sheria na haki kama vile wanasheria, polisi na wachunguzi kujifunza na kubadilishana maarifa na mawazo juu ya upatikanaji wa haki kwa kuzingatia sheria.
Muhadhara huu kwa ujumla wake unaleta umuhimu katika kukuza uwajibikaji, uwazi na uelewa wa umma kuhusu masuala ya sheria na haki nchini Urusi na hata kwa mataifa mengine.
#MSLAC
Comments
Post a Comment