
Usikate Tamaa, Haki Ipo! Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Inakuhusu! Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inalenga kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata haki zake za kisheria bila ubaguzi au vikwazo. Kupitia kampeni hii, wananchi wanapewa msaada wa kisheria kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili, ili waweze kutetea haki zao kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanzania. Huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa zinahusisha. Ushauri wa Kisheria : Kupata mwongozo sahihi juu ya hatua za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa katika masuala mbalimbali kama vile migogoro ya ardhi, ndoa, urithi, na masuala mengine ya kijamii. Mwakilishi wa Kisheria : Kupatiwa msaada wa mawakili waliobobea, ambao wanatoa usaidizi wa kisheria bila malipo kwa wale wasioweza kumudu gharama, ili kuhakikisha haki inatendeka. Elimu ya Kisheria : Wananchi wanapewa elimu ya kisheria ili wawe na ufahamu wa haki zao na wajibu wao katika jamii, na hivyo kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima. Uwezes...