Usikate Tamaa, Haki Ipo! Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Inakuhusu!
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inalenga kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anapata haki zake za kisheria bila ubaguzi au vikwazo. Kupitia kampeni hii, wananchi wanapewa msaada wa kisheria kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili, ili waweze kutetea haki zao kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Tanzania.
Huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa zinahusisha.
Ushauri wa Kisheria: Kupata mwongozo sahihi juu ya hatua za kisheria zinazopaswa kuchukuliwa katika masuala mbalimbali kama vile migogoro ya ardhi, ndoa, urithi, na masuala mengine ya kijamii.
Mwakilishi wa Kisheria: Kupatiwa msaada wa mawakili waliobobea, ambao wanatoa usaidizi wa kisheria bila malipo kwa wale wasioweza kumudu gharama, ili kuhakikisha haki inatendeka.
Elimu ya Kisheria: Wananchi wanapewa elimu ya kisheria ili wawe na ufahamu wa haki zao na wajibu wao katika jamii, na hivyo kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima.
Uwezeshaji wa Kisheria: Wananchi wanapatiwa fursa ya kuwasiliana na wataalamu wa sheria ambao wanaweza kuwasaidia kutatua changamoto zao kwa mujibu wa sheria, ili kuhakikisha kwamba matatizo yao yanatatuliwa kwa haki na usawa.
Kampeni hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote na kwamba wananchi wote wanapata fursa ya kujilinda kisheria katika changamoto zinazowakabili. Hivyo basi, usikate tamaa, haki ipo – tumia msaada wa kisheria ili kutatua changamoto zako kwa misingi ya sheria za Tanzania.
#MSLAC
Comments
Post a Comment