WAKAZI WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi leo mkoani humo. Kampeni hii inalenga kuwawezesha wananchi kwa kuwapa elimu kuhusu haki zao za kisheria na kusaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili. Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, waliongoza shughuli za utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Kliniki za kisheria ziliwekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa, ambapo wananchi walihudhuria kwa wingi na kupata fursa ya kushauriana na wataalamu wa sheria kuhusu changamoto zao, zikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, masuala ya kifamilia, na haki za kijinsia. Akizungumza na wananchi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, aliwahimiza wakazi wa Arusha kutumia fursa hii muhimu...






Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inakwenda kujenga jamii yenye uelewa mpana katika masuala ya kisheria ya ardhi,ndoa,mirathi,ukatili wa kijinsia na wosia jambo ambalo linatengeneza jamii imara yenye haki,usawa, amani na maendeleo.
ReplyDelete#MSLAC #SSH #NaipendaNchiYangu #SisiNiTanzania #SioNdotoTena #kaziiendelee #katibaNaSheria
Kampeni ya msaada wa kisheria kwa haki,usawa na maendeleo #ssh #sisinitanzania #matokeochanya #Mslac #nchiyangukwanza #kaziiendelee
ReplyDelete