VIONGOZI SONGEA NA MADABA KUPATIWA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO SEKTA YA SHERIA
Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa semina itakayotoa Elimu ya utatuzi wa Migogoro ya sekta ya Sheria kwa viongozi wa kada ya chini wa Manispaa ya Songea Mjini na wa Wilaya ya Madaba.
Akizungumza na Timu ya utoaji wa Elimu hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa ili kumaliza migogoro mbalimbali ya kisheria inayoibuka na ile iliyoibuliwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni vyema kuwapatia elimu viongozi hao ili wakabiliane nayo kuanzia ngazi za chini.
Aidha Mhe. Dkt Ndumbaro amesema mbali ya utatuzi wa Migogoro pia viongozi hao wapatiwe elimu ya uraia na Utawala bora, Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Elimu kuhusu Uchaguzi Mkuu.
Tanzania bila migogoro inawezekana..
ReplyDeleteKazi na Utu Tunasonga Mbele
Elimu hii kwa viongozi itasaidia sana katika utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala na upatikanaji wa haki kwa njia ya amani #ssh #mslac #SisiNiTanzania #NaipendaNchiYangu #matokeochanya #katibaNaSheria #NchiYanguKwanza
ReplyDeleteElimu ya msaada wa kisheria inawajengea wananchi wakizijua haki na wajibu wao. KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE#sisinitanzania#Nchiyangukwanza#matokeochanya#sisindiowajenziwatanzaniayetu
ReplyDeleteNi muendelezo wa Kampeni ya msaada wa Kisheria katika kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uelewa wa masuala ya Sheria na haki za msingi.
ReplyDelete#SisiNiTanzania
#Matokeochanya
#Katiba_sheria
#MsLAC
#DrSSH
#Tanzaniakwanza