WAKAZI WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi leo mkoani humo. Kampeni hii inalenga kuwawezesha wananchi kwa kuwapa elimu kuhusu haki zao za kisheria na kusaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili. Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, waliongoza shughuli za utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Kliniki za kisheria ziliwekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa, ambapo wananchi walihudhuria kwa wingi na kupata fursa ya kushauriana na wataalamu wa sheria kuhusu changamoto zao, zikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, masuala ya kifamilia, na haki za kijinsia. Akizungumza na wananchi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, aliwahimiza wakazi wa Arusha kutumia fursa hii muhimu...


.jpeg)

.jpeg)
Hakika hii huduma inawasaidia sanaa wananchi,Mungu awape viongozi weledi na busara na kuongeza wigo katika kuwahudumia wananchi
ReplyDeleteUkisikia huduma ya jamii ndio hii. Natamani sana na taasisi nyingine wawe kama Hawa. Tutaendelea sana.
ReplyDeleteMsaada wa kisheria Kwa jamii ni dhamira ya dhati ya serikali kutatua changamoto zinazowakabili wanainchi
ReplyDelete