MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA KUWA KITOVU CHA MSAADA KATIKA JAMII
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote Nchini, kwa moyo wake wa uzalendo na kuwatumikia Watanzania na kutokana na Maono yake aliamua kuanzisha Kampeni ya Msaada wa Kisheria kwa Watanzania.
Mnamo tarehe 27 Aprili mwaka wa 2023 , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa alizundua rasmi Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.
Kampeni hii imekuwa mahususi kwa lengo la kuwafikia na kutoa msaada wa kisheria kwa Wananchi wote buree.
Kampeni hii imehusisha utoaji wa Elimu ya kisheria na kusikiliza migogoro yote ya kisheria ikiwa ni pamoja na mirathi, ardhi, ndoa na usajili pamoja na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na mengineyo kwa Wananchi wote pasipo gharama yoyote.
Kutokea Wizara ya Katiba na Sheria ikiongozwa na Waziri Mhe. Pindi Chana imejipanga kuhakikisha wanatekeleza Kampeni hii kwa ufanisi zaidi katika kutatua changamoto za kisheria zinazowakabili Wananchi na Watanzania kwa Ujumla.
Vilevile, Wizara imejipanga na kuendelea kutoa Elimu ya Sheria kwa Wananchi ili kuwajengea uelewa mpana wa masuala ya Kisheria.
Watanzania wengi kwa makundi yote, Wanawake, Watoto, Wanaume, Wazee na Watu wenye Ulemavu wamekuwa wakitoa salamu za shukrani zao za dhati kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na namna Kampeni hii ilivyowagusa na kuwa chachu na mwarobaini wa kutibu kabisa changamoto, kero na matatizo yao kiujumla yanayohusiana na mambo ya uhitaji wa kisheria.
Hadi kufikia sasa mwezi Januari, 2024, Kampeni hii imeshafika zaidi ya Mikoa 5 ikiwemo Mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Shinyanga na Ruvuma, ambapo inakadiliwa zaidi ya Watu 25000 wamenufaika kutokana na kampeni hii.
Kampeni hii ni endelevu kwa Mikoa yote Nchi nzima.
Comments
Post a Comment