RAIS DR. SAMIA SULUHU HASSAN AANZISHA MPANGO WA KIPEKEE WA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI.



Mama Samia Legal Aid Campaign imejidhatiti kuwasaidia Wananchi kwa kuwapatia huduma ya Msaada wa kisheria maeneo walipo katika migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi utawala, matunzo ya watoto, ukatili wa Kijinsia n.k.


Kampeni  hiyo ambayo kwa sasa inatekelezwa Mkoani Singida 
Yenye malengo ya kufikia jumla ya Kata 70 na vijiji 210 vya mkoa Mkoa huo ni Azma ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuhakikisha kwamba  kila mwananchi anafahamu masuala ya kisheria ikiwemo haki na wajibu wake na kwamba kila mwananchi anaifikia haki na wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili basi waweze kufikia haki kupitia huduma za msaada wa kisheria. 

Kwa muktadha huu, Mhe. Rais ametuelekeza kuhakikisha msaada wa kisheria  unatolewa kwa wananchi wote hususani kundi la wanyonge na wasiokuwa na uwezo ili kupata haki, usawa, amani na maendeleo, Kama mnavyofahamu, nchi yetu imeendelea kupiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Haki za Binadamu na Msaada wa Kisheria nchini.


 
Hivyo, Mhe. Rais anataka kuendelea kuona kuwa Tanzania inaendelea kuwa nchi tulivu na yenye amani kwa kuwawezesha Wananchi sio tu kupata msaada wa kisheria bali kuwaelimisha kuhusu haki zao na wajibu wao kwa Taifa. Kila mmoja wetu akifahamu vizuri haki zake na wajibu wake, ndipo nchi yetu itasonga mbele kiuchumi.



Serikakali imejipanga  kikamilifu katika kuhakakisha kuwa wananchi wa Tanzania wananufaika na Mama Samia Legal Aid Campaign na kuhakikisha kuwa inawafikia wananchi wote hapa nchini.



Utekelezaji wa Kampeni hiyo umekuwa na mafanikio makubwa, tangu imeanza kutekelezwa mwezi Aprili, 2023. Hadi kufikia tarehe 30 Oktoba, 2023, Mama Samia Legal Aid Campaign imefikia mikoa mitano (05) ya  Dodoma, Manyara, Shinyanga, Ruvuma  na Simiyu ambapo jumla Halmashauri 35, Kata 397 na Vijiji/ Mitaa 1,046 imefikiwa katika utekelezaji wa Kampeni hiyo; Katika mikoa hiyo mitano, jumla ya wananchi 362,488 (Wanaume 179,874  wananwake 182,615 ) wamefikiwa kupitia elimu ya kisheria na huduma nyingine za kisheria.


#MSLAC

Comments

Popular posts from this blog