Dkt. Biteko Aitaka Tanzania Red Cross Kuendeleza Uzalendo na Umoja Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Msalaba Mwekundu

Wanachama na wadau wa Shirika la Msalaba mwekundu nchini (Tanzania Red cross Society) wametakiwa kusimamia kanuni saba (7) zinazoongoza shirika hilo ambazo ni ubinadamu, uadilifu, kutopendelea, uhuru, kujitolea, umoja, na umataifa ambazo kimsingi zinafundisha na kuzalisha wananchi wenye uzalendo

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Mashaka Biteko alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya Red cross Duniani ambayo kitaifa yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya kimataifa wa Jakaya Kikwete (JKICC) jijini Dodoma ambapo katika maelezo yake ameipongeza Tanzania Red cross Society kwa namna wanavyokuwa mstari wa mbele kwenye kuthamini uhai wa binadamu wengine jambo ambalo ni la kuigwa si tu Tanzania bali Afrika na Dunia nzima kwa ujumla wake
Amesema hapa nchini Red cross imekuwa ikidhihirisha jambo hilo kwa muda mrefu, ambapo kwa siku za karibuni miongoni mwa matukio ya kukumbukwa ushiriki wao ni pamoja na majanga ya mafuriko yaliyotokea Hanang mkoani Manyara, UVIKO-19, na majanga mengine ikiwemo kipindupindu, mafuriko ya Rufiji nk, mchango ambao unathaminiwa kwa kiasi kikubwa na serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa yeye (Rais) amewahi kutoa chetu maalumu kwa Red cross kudhihirisha kuwa ushirikiano baina ya serikali na Red cross
utakuwa endelevu Katika hatua nyingine Dkt. Biteko ametoa wito kwa wanachama wote wa Red cross nchini kutambua kuwa mwaka huu (2024) ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo wanachama hao wanaombwa kujitolea kuendelea kuiombea nchi amani na utulivu ili chaguzi zijazo zipite kwa amani
Amesema anatambua kuwa Red cross haihusiki na masuala ya siasa lakini ni vyema wakajipanga kutoa huduma kwenye mikutano ya siasa, na kwamba wakati wanatimiza majukumu yao wasisite kuimiza amani na upendo miongoni mwa Watanzania, kwani chaguzi hizo hazipaswi kuleta mgawanyiko wa aina yoyote i
le iwe ya Dini, kabila au ukanda
Aidha, Dkt. Biteko amesisitiza
kuwa Tanzania inapaswa kuendelea kuwa Taifa lenye umoja, ustaarabu, kuheshimiana, kuthaminiana na kujaliana ili urithi tuliorothishwa kutoka kwa waasisi wetu uendelee vivyo hivyo kwa vizazi vya sasa na vijavyo

#MSLAC

Comments

Popular posts from this blog