Uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria uliofanyika mjini Njombe ulihudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Pindi Chana, Naibu Waziri Jumanne Abdallah Sagini, na Katibu Mkuu wa Wizara, Bi. Marry Makondo. Wakiwa kwenye mazungumzo, viongozi hawa walijadili jinsi wananchi wanavyoweza kufaidika na kampeni hii ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mama Samia. Kampeni hii inalenga kutoa huduma za kisheria kwa wananchi, kuboresha upatikanaji wa haki na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kisheria.
Huduma ya Msaada wa Kisheria Yafika Halmashauri ya Rorya, Mara: Wananchi wa Kata ya Bukura, Kijiji cha Bubombi na Kirongwe Wapata Mafunzo Kuhusu Haki na Sheria Muhimu Katika muendelezo wa utekelezaji wa utoaji huduma ya msaada wa kisheria, timu ya afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Rorya, Mara, ilitua katika kata ya Bukura, kijiji cha Bubombi na Kirongwe kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwajulisha juu ya uwepo wa dawati la msaada wa kisheria ndani ya halmashauri yao. Wananchi walipata fursa ya kujuzwa kuhusu namna dawati hili linavyofanya kazi na umuhimu wake katika utoaji wa haki. Wakati wa ziara hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa kwa kina, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi, Sheria ya Ndoa, Mirathi na Wosia, Ukatali wa Kijinsia, Utatuzi wa Migogoro, na Haki za Watoto. Huduma hii ni sehemu ya juhudi endelevu za kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu na msaada wa kisheria ili kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii zao.

Comments
Post a Comment