
Je, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Inatoa Msaada wa Namna gani Kwa Watanzania? Kampeni ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mhe.Rais.Dkt.Samia Suluhu Hassan inagusa maeneo mbalimbali nchini Tanzania kwa lengo la kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi. Maeneo muhimu ambayo kampeni hii inagusa ni pamoja na: Elimu ya Kisheria :MSLAC inatoa elimu ya kisheria kwa wananchi kuhusu haki zao za kikatiba na sheria zinazowalinda, ikiwemo sheria za ardhi, haki za wanawake, watoto, na makundi maalum. Utoaji wa Huduma za Kisheria : Kampeni inawafikia wananchi kwa kuwapatia huduma za msaada wa kisheria, hasa wale wasio na uwezo wa kumudu gharama za kisheria. Hii inahusisha msaada wa kisheria wa bure kwa wananchi katika migogoro mbalimbali. Ulinzi wa Haki za Wanawake na Watoto : Moja ya malengo makubwa ya kampeni ni kulinda haki za wanawake na watoto, kwa kutoa msaada katika kesi zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia, haki za urithi, ndoa, na talaka. Kusaidia Watu Wa...