KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAFANA KISAWASAWA NA KIBEREGE

Katika kilele cha Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, tulifanikiwa kufikisha elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi wa kata ya Kisawasawa katika vijiji vya Kisawasawa, Ichonde, na Kanoro, ndani ya Halmashauri ya Mji wa Ifakara. Kampeni hii iliwaleta pamoja wataalam wa kada mbalimbali, wakiwemo mawakili, wanasheria, maafisa maendeleo ya jamii, maafisa wa dawati la msaada wa kisheria, dawati la jinsia, paralegal, pamoja na maafisa ustawi wa jamii. 

Lengo kuu la kampeni lilikuwa ni kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya msaada wa kisheria, haki zao kikatiba, na huduma wanazoweza kupokea kutoka kwa mamlaka husika. Juhudi hizi zimekuwa chachu ya kuimarisha upatikanaji wa haki kwa makundi yote ya jamii, hususan wale walioko maeneo ya vijijini ambao mara nyingi hukosa fursa ya kupata huduma za kisheria.  

 


Kwa upande wa kata ya Kiberege, mwitikio wa wananchi ulikuwa mkubwa. Idadi kubwa ya wakazi walijitokeza kushiriki na kupokea elimu hii muhimu. Kupitia kampeni hii, wananchi walielimishwa kuhusu namna ya kupata msaada wa kisheria, jinsi ya kushughulikia migogoro ya kifamilia, ardhi, mirathi, na masuala mengine ya kijamii.  

 

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia inadhihirisha dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha haki inapatikana kwa kila Mtanzania bila ubaguzi. Ushirikiano wa wataalam waliobobea na watoa huduma wa ngazi za chini umechangia kufanikisha malengo ya kampeni hii.  

 

#MSLAC #KaziIendelee

Comments

  1. Hongera Kwa kuhitimisha kampeni hii mkoa wa Morogoro, Wananchi wengi wamefaidika kupata Elimu na msaada wa kisheria.
    #SisiNiTanzania
    #HayaNdioMatokeoChanya+
    #Tanzaniakwanza
    #MSLAC
    #Katiba_sheria
    #DrSSH

    ReplyDelete
  2. pongezi kwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa dr Samia Suluhu Hassan kwa kampeni ya msaada wa kisheria bure ambao umekuw ni msaada n tumaini kubwa kwa watanzania #SisiNiTanzania #SSH #mslac #HayaNdioMatokeoChanyA #SioNdotoTena

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog