KUANDIKA WOSIA SIO KUJICHULIA KIFO-MSLAC
Elimu ya usimamizi wa mirathi imeendelea kutolewa na timu ya wataalamu wa Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambapo wananchi wametakiwa kuzidi kuwa na tabia ya kuandika wosia ili kuondoa sintofahamu kwa ndugu wanaobaki pindi wanapofariki.Akizungumza mratibu wa mradi huo Halmshauri ya Tanganyika Pendoveera Nyanza amewataka wakazi wa Kata za Karema na Kapalamsenga zilizopo katika mwambao za Ziwa Tanganyika mkoa mkoani Katavi, kuondoa dhana potofu ya kuwa endapo ataandika wosia mapema ni kujichulia kifo.
Kwa upande wake Christina Ngalikiliwi kutoka dawati la Jinsia na watoto halmashauri ya Tanganyika amewataka wanandoa kuacha kufanyiana ukatili kwani matendo hayo hupelekea familia kusambaratika hali inayozalisha watoto wa mtaani.
Aidha amekemea matendo ya ubakaji na ulawiti yanayofanywa na watu wazima dhidi ya watoto kwani hukatisha ndoto za watoto na kuwakosesha haki zao za msingi.
Mussa Kassim mkazi wa Karema amekiri uwepo wa matendo ya ukatili vikiwemo vipigo ndani ya ndoa ambavyo hutokana na wao kunyimwa unyumba na wake zao pindi wanapowahitaji.
Kupitia kampeni hiyo wananchi wote wa Kata hizo wenye kuhitaji kutatuliwa matatizo yanayohitaji msaada wa kisheria walipata fursa ya kusikilizwa na kutatuliwa changamoto zao nyingi zikiwa za wanaume na wanawake kufanyiwa ukatili, mirathi, masuala ya uraia na kero za ardhi.
Tunamshukru sana Mh Rais samia kwa kuweza kuanzisha huu mpango chini ya wizara ya katiba na sheria kwani umekua msaada mkubwa sana kwetu sisi wananchi wa hali ya chini kwani ilikua ngumu sana kupata usaidizi huu kwani ilikua ghalama sana kukutana na wanasheria lakini saivi tunapata huu msaada hapa hapa mtaani kwetu
ReplyDelete#mslac
#sisinitanzania
#katibanasheria
#ssh
#kaziiendelee
Huduma hii ni tiba tosha kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kugharamia kuendesha kesi mahakamani kupata haki bure kabisa
ReplyDelete#mslac
#sisinitanzania
Ukosefu wa elimu ya sheria unasababisha migogoro mingi. Wananchi wanahitaji elimu ya kisheria ili kulinda haki zao na kuepuka dhuluma. Serikali na wadau waendelee kuelimisha jamii🇹🇿
ReplyDelete#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Hakika haya ni matokeo chanya ya nchi yetu ya Tanzania @ssh @sisinitanzania @Mslac #siondototena #nchiyangukwanza #naipendanchiyangu #Mslac #ssh #kaziiendelee
Delete