KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YAENDELEA KUTOA HUDUMA KATIKA MKOA WA LINDI, HALMASHAURI YA MTAMA, KATA YA MANDWANGA
Mtama, Lindi – Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign - MSLAC) imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kuwapatia wananchi elimu ya msaada wa kisheria katika Mkoa wa Lindi, hususan katika Halmashauri ya Mtama, Kata ya Mandwanga.
Katika zoezi hili muhimu, wananchi wa Kata ya Mandwanga walipata fursa ya kuelimishwa juu ya haki zao za kisheria, taratibu za kutatua migogoro, pamoja na njia mbadala za usuluhishi ili kuepusha migogoro inayoweza kuleta madhara katika jamii. Timu ya wanasheria na wataalamu wa msaada wa kisheria ilisikiliza changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi na kutoa ushauri wa kisheria ili kuhakikisha haki inapatikana kwa kila mmoja.
Masuala yaliyotiliwa mkazo katika kampeni hii ni pamoja na migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, ukatili wa kijinsia, masuala ya ajira, na haki za makundi maalum kama wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu. Pia, wananchi walihamasishwa kuandika wosia na kutumia njia za upatanisho, maridhiano, na usuluhishi ili kuepusha kesi zisizo za lazima mahakamani.
Wananchi waliohudhuria wameipongeza serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaletea huduma za msaada wa kisheria karibu na maeneo yao. Wameeleza kuwa kampeni hii ni msaada mkubwa kwao kwani wengi walikuwa hawajui taratibu za kisheria katika kutatua changamoto zao.
Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia itaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu na huduma muhimu za kisheria kwa lengo la kujenga jamii yenye haki na usawa.
msaada wa kisheria kwa haki, usawa amani na maendeleo #MSLAC #SSH #SisiNiTanzania #SioNdotoTena #NaipendaNchiYangu #kaziiendelee #katibaNaSheria #matokeochanya
ReplyDeleteHakika MSLAC ni tumaini jipya kwa watanzania wanyonge walipoteza haki zao.
ReplyDelete#SisiniTanzania
#nchiyangukwanza
#matokeochanya