MZAMIRU YASSIN, MCHEZAJI WA SIMBA SC, APATA MSAADA WA KISHERIA KUPITIA KAMPENI YA MAMA SAMIA – KIGAMBONI, DAR ES SALAAM
Mchezaji wa klabu ya Simba SC, Mzamiru Yassin, amejitokeza katika Kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia iliyoendelea kutolewa bure kwa wananchi katika eneo la Kigamboni, Dar es Salaam.
Mzamiru alipata nafasi ya kupokea msaada wa kisheria kupitia kampeni hii inayoratibiwa chini ya Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria. Mchezaji huyo amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuandaa huduma hii muhimu inayowasaidia wananchi wote, wakiwemo wanamichezo, kupata haki zao kwa njia halali na salama.
Kupitia tukio hilo, Mzamiru amehamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kufaidika na huduma hizi zinazotolewa bure, akisisitiza kuwa msaada wa kisheria ni haki ya kila raia na msingi muhimu wa amani, usawa na maendeleo.Kampeni hii imeendelea kuvutia watu kutoka makundi mbalimbali ya jamii, ikiwa ni uthibitisho wa mafanikio ya dhamira ya Mama Samia katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote, bila ubaguzi.
📍Kigamboni leo – haki inatendeka, Tanzania inasonga mbele!
Kampeni ya huduma ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni kombilio la wengi katika kupata msaada wa Kisheria
ReplyDelete