Huduma ya Msaada wa Kisheria Yafika Halmashauri ya Rorya, Mara: Wananchi wa Kata ya Bukura, Kijiji cha Bubombi na Kirongwe Wapata Mafunzo Kuhusu Haki na Sheria Muhimu Katika muendelezo wa utekelezaji wa utoaji huduma ya msaada wa kisheria, timu ya afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Rorya, Mara, ilitua katika kata ya Bukura, kijiji cha Bubombi na Kirongwe kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwajulisha juu ya uwepo wa dawati la msaada wa kisheria ndani ya halmashauri yao. Wananchi walipata fursa ya kujuzwa kuhusu namna dawati hili linavyofanya kazi na umuhimu wake katika utoaji wa haki. Wakati wa ziara hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa kwa kina, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi, Sheria ya Ndoa, Mirathi na Wosia, Ukatali wa Kijinsia, Utatuzi wa Migogoro, na Haki za Watoto. Huduma hii ni sehemu ya juhudi endelevu za kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu na msaada wa kisheria ili kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii zao.
Popular posts from this blog
MSLAC YAZIDI KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI KWA WANANCHI NCHINI TANZANIA
Kampeni ya Msaada wa Kisheria nchini Tanzania imezidi kushika kasi, ikiwalenga wananchi wa kawaida kwa kuwapatia elimu ya sheria na msaada wa kisheria bure. Kampeni hii, inayoendeshwa chini ya mwamvuli wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Samia (MSLAC), inalenga kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa wote, hususan kwa makundi yaliyo pembezoni kama wanawake, watoto, na watu wa kipato cha chini. Tangu kuanzishwa kwake, kampeni hii imefanikiwa kuwafikia wananchi wengi katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Shinyanga, Kisarawe, Morogoro, Iringa, Songwe, na Mara. Katika maeneo haya, wananchi wamepata mafunzo kuhusu sheria za ardhi, mirathi, ndoa, kesi za jinai, ukatili wa kijinsia, mikataba ya ajira, na umuhimu wa kuandika wosia. Aidha, kampeni hii imehimiza matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro, kama usuluhishi na maridhiano, ili kupunguza mrundikano wa kesi mahakamani. Kwa kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria, pamoja na taasisi mbalimbali kama Tanganyika Law Society (...
VIONGOZI SONGEA NA MADABA KUPATIWA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO SEKTA YA SHERIA
Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa semina itakayotoa Elimu ya utatuzi wa Migogoro ya sekta ya Sheria kwa viongozi wa kada ya chini wa Manispaa ya Songea Mjini na wa Wilaya ya Madaba. Akizungumza na Timu ya utoaji wa Elimu hiyo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa ili kumaliza migogoro mbalimbali ya kisheria inayoibuka na ile iliyoibuliwa na Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ni vyema kuwapatia elimu viongozi hao ili wakabiliane nayo kuanzia ngazi za chini. Aidha Mhe. Dkt Ndumbaro amesema mbali ya utatuzi wa Migogoro pia viongozi hao wapatiwe elimu ya uraia na Utawala bora, Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na Elimu kuhusu Uchaguzi Mkuu.



#miminamuungano #sisinitanzania #Mslac #katibanasheria
ReplyDelete