SALAM ZA RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA WA TANGANYIKA, WAKILI HAROLD SUNGUSIAKATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA, TAREHE 1 FEBRUARI, 2024  VIWANJA VYACHINAGALI DODOMA.

 Nianze kwa kumshukuru Mwenyenzi Mungu, mwingi wa rehma na mwenye fadhila tele kwakutuwezesha sote kuuona mwaka 2024, tukiwa na afya njema. Naomba uniruhusu kuishukuru Mahakama ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutambua mchango wa Chama chaWanasheria Tanganyika


kama mmoja wa wadau muhimu katika sekta ya haki hapa nchini kwa kutupatia nafasi yakushiriki katika maadhimisho haya ya kihistoria ya siku ya sheria nchini.

 

Mhe. mgeni rasmi,

Huu ni mwaka wa kipekee kwa Chama Cha Wanasheria Tanganyika kwa kuwa kinatimizamiaka 70 tangu kuanzishwea kwake. Tunafahamu sote kuwa Chama hiki kilianzishwa kwa sheria yaani The Tanganyika Law Society Ordinance ya mwaka 1954 Sura ya 344 na sheria hiyo ikaanzakutumika rasmi tarehe 1 Januari 1955. Baada ya Uhuru, Sheria iliendelea kutumika na hadi sasa chama hiki kinaendelea kuongozwa na sheria hii pamoja na kufanyiwa marekebisho kwamiaka tofauti, yaani Tanganyika Law Society Act, Cap 307

R.E. 2002. Chama hiki kilianzishwa kwa malengo mbali mbali yaliyobainishwa katika kifungu cha 4 cha sheria hii tajwa, na baadhi ya malengo hayo ni kuisaidia Serikali, Bunge na Mahakama katika maswala yote yanayoathiri sheria, kulinda na kusaidia umma katika maswala yote yakisheria; pamoja na kuwalinda na kuwasaidia wanachama wake katika maswala yanayogusa hali za utendaji kazi wao katika maswala ya sheria na taaluma ya sheria.

 

Mhe. mgeni rasmi,

Kauli mbiu ya wiki ya sheria kwa mwaka huu ni “UMUHIMU WA DHANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA: NAFASI YA MAHAKAMA NA WADAU KATIKA KUBORESHA MFUMO JUMUISHI WA HAKIJINAI.”

 

Kwa kuendana na kauli mbiu ya wiki ya sheria ya mwaka huu, ni dhahiri kuwa Chama chaWanasheria Tanganyika kimekuwa mdau mkubwa na muhimu wa masuala ya haki na kimekuwamstari wa mbele kushirikiana na mihimili mitatu ya dola yaani Serikali, Bunge na Mahakama,taasisi mbali mbali na wadau wa haki kuhakikisha kuwa kinalinda na kutetea haki kwa maslahi yaumma.


Mhe. mgeni rasmi,

Kwa kuwa dhima ya Maadhimisho haya ni haki Jinai, naomba uturuhusu tuzungumzie mambomanne makubwa na ambayo ni yale tu yanayohusu haki jinai katika ushirikiano baina ya Chama cha Mawakili Tanganyika na Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. mgeni rasmi,

I: Nafasi ya TLS Katika Kutekeleza Mapendekezo ya Tume ya Kuboresha Mifumo na Taasisiza Haki Jinai

Sote tunafahamu kuwa mnamo tarehe 31 Januari mwaka 2023 Rais wetu mpendwa, Mheshimiwa, Dr. Samia Suluhu Hassan aliteua Tume ambayo aliipatia kazi ya kukusanya maoni na kisha kuwasilisha mapendekezo ya namna ya kuboresha na kurekebisha mifumo nataasisi za haki jinai nchini, iliyoongozwa kwa umahiri na ufanisi mkubwa na Mwenyekiti wakeMheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Othman Mohamed Chande pamoja na Katibu Mkuu Kiongozimstaafu, Balozi Ombeni Yohana Sefue, akiwa makamu mwenyekiti na wajumbe wengine Tisa akiwemo Rais Mstaafu wa Tanganyika Law Society, Profesa Edward Hosea Gamaya. Tume ya haki jinai ilitoa taarifa yenye mapendekezo mbalimbali ya namna ya kuboresha mifumo nataasisi za haki jinai mnamo mwezi Julai, 2023. Tunampongeza sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka kipaumbele katika kuboresha mifumo ya haki jinai kwa ustawi wa taifa letu. Hii haikuja kama bahati mbaya bali udhihirisho wa kupenda mfumo wa hakijinai utoe haki. Tarehe 25 Agosti, 2021 Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alipohutubia katika ufunguzi wa kikao cha Maafisa wakuu waandamizi waJeshi la Polisi na makamanda wa Polisi wa mikoa/vikosi Dar es Salaam alizungumza mambomazito sana kuhusu haki jinai. Naomba ninukuu baadhi ya kauli zake. “Kwa zile kesi ambazo mna hakika upelelezi hautokamilika hao watu watolewe, wakafaidi huru wao wakiwa nje kamakesi haina mwelekeo basi hao watu watolewe lakini zile kesi ambazo mna uhakika


upelelezi utatimia basi ziharakishwe’’  “Kwa upande mwingine Mwanadamu ni Mwanadamu na ana uhuru wake naomba mkae na wadau wengine muangalie uwezekano wa kurekebisha sheria ya kumuweka mtu mahabusu”…. “haki kwa jamii ndiyo wajibu wetu mkubwa;” …. “jeshila polisi mnashutumiwa kwa kutofanya haki kwa jamii’’ …"tuko hapa kuhudumia watu na sikudidimiza watu”… “naomba sana ndugu zangu tendeni yaliyo haki.”

Kwa kuzingatia nukuu hizo za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni dhahiri kuwa kilaMtanzania mpenda haki ataungana nasi katika kuhakikisha kuwa nia njema, utashi na juhudi zaMh. Rais katika kuboresha na kuimarisha mifumo na taasisi za haki jinai nchini zinatekelezwa kwatija na ufanisi mkubwa. Nasi tunauhakikishia umma kuwa Chama cha Wanasheria Tanganyika kimejizatiti kimkakati ili kuhakikisha kwamba kinatoa mchango wa kitaalam kadiri iwezekanavyona kama itakavyohitajika ili kutekeleza kwa tija na ufanisi mapendekezo yaliyotolewa na Tume yaHaki Jinai. Baadhi ya mambo ambayo tumekusudia kuyafanya ni Pamoja na:-

a)            kuendelea kuboresha mahusiano mazuri baina ya Chama Chetu na wadau mbalimbaliwa haki jinai hususan Mahakama, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali; Ofisi ya Taifa ya Mashtaka; Taasisi ya Kuzuia naKupambana na Rushwa; na Wadau wengine katika kuhakikisha kuwa Mchango waWanachama wetu ambao ni Mawakili wa Kujitegemea, Mawakili wa Serikali, Mahakimu na Majaji kwa umoja wetu na kwa nafasi zetu tunasimamia kwa dhatiupatikanaji wa haki jinai.

b)            Chama kitaendelea kuhimiza mabadiliko au maboresho ya kila kipengele katika mnyororo wa haki jinai yaani kuzuia uhalifu; kung’amua makosa; ukamataji; upelelezi;uendeshaji wa mashtaka; utetezi; usikilizwaji wa mashauri ya jinai; utoaji wa hukumu; utekelezaji wa adhabu; urekebishaji wa wahalifu na urejeshaji wa raia waliojirekebishwa kwa umma. Chama kitapitia sera, Mikakati na


sheria mbalimbali zinazogusa haki jinai na kuwasilisha mapendekezo yetu katika ngazi husika hii ikiwa ni pamoja na kufanya ufuatiliaji (monitoring) ya utekelezwaji wamapendekezo hayo.

c)            Vile vile chama chetu kimejipanga kuendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheriakwa Wananchi wasiojiweza kiuchumi kumudu gharama za kumlipa wakili ili kuwakilishwa Mahakamani katika mashauri yanayowakabili, na pia wanachama wetu ambao ni mawakili wakujitegemea wataendelea kupokea mashauri ya kesi za jinai wanayopangiwa na Mahakama ili kuweza kuwawakilisha watuhumiwa mbalimbali wakesi za jinai ambao wamekosa uwakilishi Mahakamani; TLS tumekuwa tukitoa msaada wakisheria kwa mujibu kifungu namba 10 cha Sheria ya Msaada wa Kisheria ya mwaka 2017 (The Legal Aid Act 2017). Msaada huu utakuwa na msukumo mkubwa kama tutafanyakazi hii kwa kushirikiana kwa ukaribu na kwa pamoja na wadau wote wa haki;tunaipongeza wizara ya Katiba na Sheria kwa juhudi nyingi za kutoa msaada wa kisheria kupitia, mpango wa Mama Samia Legal Aid Campaign

d)            Chama chetu pia kimejipanga kuendelea kutoa elimu kwa Umma kuhusu maswala yahaki jinai hii ni pamoja na haki za mtuhumiwa, dhamana, ushahidi, pamoja na taratibuza uendeshaji wa mashtaka.

e)            Hali kadhalika, Chama chetu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa haki jinai kitaendelea kujenga na kuimarisha uwezo wa wanataaluma na Taasisi mbalimbali za Serikali, Mahakama na Wadau wengine kuhusu masuala yote yanayohusu haki jinai na uimarishaji wa taasisi na mifumo ya haki jinai ili kufanikisha utekelezaji wamapendekezo yote yaliyotolewa na Tume ya haki jinai.

Chama cha Wanasheria Tanganyika kinaamini kuwa endapo mapendekezo yaliyotolewa na Tumeya Haki jinai yatafanyiwa kazi ipasavyo, basi tutakuwa


na taifa lililopiga hatua muhimu kwenye kujali na kusimamia misingi ya haki na kuhakikisha kuwahaki inapatikana na inadhihirika kutendeka.

 

Mhe. mgeni rasmi,

II: Mchango wa TLS Katika Kusaidia Wananchi Watuhumiwa Wasiokuwa na Uwezo wa Kuwalipa Mawakili

Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika wameendelea kuaminiwa na Mahakama na kukabidhiwa majadala ya kesi za jinai ili kuwawakilisha watuhumiwa wasio na uwezokumudu gharama za wakili. Kwa mwaka 2023, jumla ya mawakili 398 kutoka kwenye Matawi yetu(chapters 21) walipewa kazi ya kuwawakilisha watuhumiwa katika mashtaka yanayowakabili.Pamoja na kazi kubwa inayofanywa na Mawakili hawa kwa moyo wa kijitolea, bado wamekutana na changamoto mbalimbali ambazo tunaamini kuwa Mahakama inaweza kuzitatua.

Miongoni mwa changamoto kubwa ni hizi zifuatazo:-

a)            Malipo yasiyowiana na ukubwa/uzito wa kazi

Mawakili wanapokuwa wamekabidhiwa jalada, wamekuwa wakipokea mkupuo wastani wa Shilingi laki moja (100,000/- ) hadi laki tatu (300,000/-) kwa ajili ya kuendesha kesi za watuhumiwa wa makosa ya jinai, ambapo ulipaji wa malipo hayo kwa wakili hutegemea tathmini inayofanywa na Jaji husika kwa kadiri anavyoona inafaa. Mara nyingi mashauri haya huendeshwa mfululizo kwa zaidi ya siku tatu hadiwiki wiki mbili. Kiwango hiki cha malipo ni kidogo mno na mara nyingi huwa hakikidhihata gharama za usafiri kwa wa wakili kwenda Mahakamani. Vilevile, kiwango hiki hakilingani na viwango ambavyo Waendesha Mashtaka wanacholipwa. Kwa ujumla tunaomba sana posho watakazolipwa mawakili wa kujitegemea wakati wa kusimamiahizi kesi zizingatie swala zima la kupanda kwa gharama za Maisha kama vile nishati ya


magari; malazi au/na posho za kijikimu pamoja na fidia ya muda wa mawakili.

b)            Ucheleweshaji wa malipo ya wakili

Pamoja na kwamba Mawakili wanapewa kiwango kidogo cha malipo, pia limekuwepotatizo la ucheleweshaji wa malipo hayo pindi wakili anapomaliza kuwakilisha mtuhumiwa katika kesi aliyopewa kuiendesha. Hali hii huwavunja moyo Mawakili, tunaiomba Mahakama iweke ukomo kwa muda wa kuwalipa Mawakili na ikibidi,Mawakili wapewe posho ya awali ya kujikimu mara tu wanapokabidhiwa jalada ya mtuhumiwa.

c)            Ucheleweshwaji wa cause list na majalada ya kesi kwa mawakili Kazi ya kumteteamtuhumiwa inahitaji maandalizi ya kutosha. Hata hivyo, mara kwa mara kumekuwana changamoto ya Mawakili kutokupewa cause list na majalada ya kesi mapemaili waweze kujiandaa vizuri na mashauri hayo. Tunaiomba Mahakama iharakisheupatikanaji wa cause list na irahisishe upatakinaji wa Majalada mapema si chini ya wiki mbili kabla ya tarehe za shauri husika ili mawakili wapate muda wa kutosha kujiandaa na kutoa uwakilishi wenye tija kwa watuhumiwa.

d)            Kukosekana kwa baadhi ya nyaraka muhimu kwenye jalada, na makosa ya kiuchapaji.

Vilevile kumekuwepo na baadhi ya majalada ambayo Wakili hukabidhiwa pasipokuwana baadhi ya nyaraka muhimu. Jambo hili huleta mivutano ya mara kwa mara kati ya wanachama wetu na upande wa Jamuhuri pindi wakili anapoomba kupewa nakalavivuli za nyaraka halisi zinazokusudiwa kutolewa Mahakamani kama maelezo ya onyo au maelezo ya ungamo. Tunaomba Mahakama iongeze nyezo za uhakiki wa nyarakazinazokabidhiwa kwa wakili.


e)            Mawakili wa kujitegemea kutoshirikishwa katika bajeti na vikao vya maandalizi ya sessions

Chama kinaomba uongozi wake katika ngazi za Chapters uhusishwe kwa uwazi katika vikao vya maandalizi ya bajeti na vikao vya Mahakama vya kusikiliza mashauri(sessions)

f)             Watuhumiwa wanaotoka kwenye magereza yaliyo mbali na Mahakama kuletwa kwakuchelewa na hivyo kuwanyima mawakili muda mzuri wa kukutana nao na kuongeanao kabla ya kesi kuanzaTunaiomba Mahakama iratibu mawasiliano kati ya wakili na mtuhumiwa kwa kuwasiliana na Mageraza, kutoa nauli za wakili kutembeleamtuhumiwa; na pia kuhimiza Magereza kuwawahisha Watuhumiwa Mahakamani na kutoa muda wa kutosha kwa Wakili kuongea na Mtuhumiwa husika kabla ya usikilizwajiwa kesi kuanza.

Mbali na changamoto hizi zinazotokana na kupatiwa mashauri ya jinai Mawakili wetuwamekuwa wakikumbana na kero mbalimbali katika utendaji kazi wao hususan wanapokuwaMahakamani na kwenye vituo vya Polisi na Magereza. Changamoto hizo ni kama vile;

a)            Mahakama nyingi (ukiacha vituo jumuishi vya haki) kutokuwa na chumba maalum chakusubiri kuitwa kwenye kesi za wateja wao na hivyo kufanya wawe wanazagaa ndani ya viunga vya Mahakama

b)            Mfumo wa e-filing kutokuwa rafiki. Mara kwa mara mtandao na mfumo kwa ujumla huwa haupatikani hewani na kuchelewesha kukusanya nyaraka za kesi kwa wakati. Vile vile wakati wa kufile subsequent documents mara nyingi umekuwa unashindwa kugenerate namba ya malipo (control number).

c)            Baadhi ya Mahakimu au Majaji wanalalamikiwa kukiuka maadili na walalamikaji kutishiwa pindi wanapotoa taarifa za ukiukwaji wa maadili

d)            Uhairishaji wa kesi pasipo Wakili kupewa taarifa


e)            Kutozingatia udharura wa mashauri ya muhimu mathalani kesi kama za habeas copus huweza kusikilizwa hadi mwezi mmoja na hivyo kusababisha sheria kuendeleakuvunjwa

f)             Kesi kutokupangwa kwa wakati husababisha mawakili kupoteza muda mwingi Mahakamani. Kwa mfano, kesi inapangwa saa tatu asubuhi, lakini ikaitwa saa nanemchana. Hii humsababishia wakili na mteja wake kupoteza muda mwingi ambao wangeweza kuutumia kwa shughuli zingine za uzalishaji.

g)            Jeshi la Polisi kutowapa ushirikiano mawakili na mara nyingine kuwachanganya mawakili kwenye tuhuma za wateja wao. Kuna wakati, Mawakili wamekuwa wanajumuishwa katika tuhuma za wateja wao pindi wanapokwenda kuwaona namara nyingine hata kuwakatalia kuwaona wateja wao wanapokuwa wamekamatwa polisi.

h)            Changamoto ya kubadilisha kesi kwa watuhumiwa na kuwabambika makosa yasiyo nadhamana kisheria

i)              Kesi nyingi za watu wanaojifanya ni Mawakili (Vishoka) ambazo zimeripotiwa polisi bado hazijafikishwa Mahakamani, hivyo kuendelea kuidhalisha tasnia yetu

j)             Urasimu kwenye Magereza pindi Mawakili wanapokwenda kuonana na wateja wao waliovizuizini.

Mhe. mgeni rasmi,

Kutokana na changamoto hizi, ni rai yetu kwamba Mahakama, Jeshi la Polisi na magerezawashughulikie changamoto hizi ili kuweka mazingira wezeshi na rafiki kwa Mawakili kufanya kaziya kuimarisha haki jinai na tunapendekeza kwamba;

a)            Mahakama iendelee kuuboresha wa e-filing ili uwe rafiki zaidi na usaidie upatikanaji wa haki usiochelewa


b)            Kesi zipangwe kwa muda maalumu na Mahakama izingatie muda huo. Teknolojiaitumike kuwapa taarifa Mawakili na wateja wao ili kupunguza gharama

c)            Kila Mahakama iwe na chumba maalumu kwa Mawakili kusubiria kuitwa kwenyemashauri ya wateja wao sababu Mawakili ni ma Afisa wa Mahakama.

d)            Kuwe na miongozo ya kuwalinda watoa taarifa (whistle blower protection guidelines) za kuwalinda Mawakili na watoa taarifa wengine dhidi ya ukiukwaji wa maadiliMahakamani.

e)            Jeshi la Polisi lifanye kazi kwa karibu na Chama cha Wanasheria Tanganyika katika ngazi zote ili kupunguza na mwisho kuondoa kabisa mivutano na visa dhidi ya Mawakilina Polisi. Ikiwa ni pamoja na kukomesha kabisa tabia ya kuwachanganya Mawakili katika tuhuma za wateja wao.

f)             Tunaomba Jeshi la Magereza kwa uratibu wa Mahakama liweke dawati maalumu la mapokezi la Mawakili ili kuweza kuwasaidia kuonana na wateja wao magerezani pasi na usumbufu ila kwa kuzingatia kanuni zote za kiusalama.

 

Mhe. mgeni rasmi,

III: Wajibu wa TLS Katika Kusimamia Utawala wa Sheria na Kupambana Na Uhalifu Mamboleo na Unaovuka Mipaka ya Nchi

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinafuatilia kwa karibu matukio yanayotokea ulimwenguni yanayogusa haki jinai na kupevuka kwa uhalifu unaovuka mipaka ya nchi. Maathalan, makosa ya jinai za kimataifa (international crimes); Uhalifu unaovuka mipaka(transnational crimes); Uhalifu unaotumia teknolojia (Cyber-based crimes); Uhalifu wa Kifedha(Financial Crimes) na kukua kwa teknolojia na akili bandia (Crimes and Artificial Intelligence),n.k. na jinsi haya yote yanavyoathiri tasnia ya sheria hasa sekta


ndogo ya haki jinai. Kwa ujumla kuongezeka kwa maendeleo ya kisayansi na muingiliano watamaduni, kumeibua changamoto nyingi ambazo zinazikumba nchi mbalimbali ulimwenguniikiwemo Tanzania. Suala la utakatishaji wa pesa (Money Laundering), usafirishaji haramu waBinadamu (Human Trafficking), utumwa mamboleo (Modern Slavery), Ngono za mitandaoni (Cyber-sex); makosa ya mitandaoni (Cyber enabled Crimes- ikiwemo cyrpto currency relatedoffences), ufadhili wa ugaidi (Terrorist Financing) na makosa mengine kama hayo yamesababishanchi mbalimbali kuchukua hatua tofauti tofauti za kimkakati. Hata hivyo imekuwa vigumu sanakuweka uwiano katika kudhibiti uhalifu huo kwa upande mmoja na kulinda haki za msingi zaBinadamu kwa upande wa pili.

 

Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinafahamu kuwa nchi yetu Tanzania iliwekwa kwenyeorodha ya nchi zilizoko kwenye uangalizi tangu Oktoba 2022 katika orodha na Financial ActionTask Force (FATF). Hivi sasa taifa letu katika utekelezaji wa mapendekezo yale 40 ili nchi yetu iweze kujinasua katika odhodha hiyo ya kijivu (grey list). Tunatoa wito kwa wanachama wetu kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika nchi yetu ili kuhakikisha kuwa biashara yetuna huduma zetu za uwakili zinafanyika kwa kufuata kanuni na sheria zilizopo. Hii itasaidiakupunguza uwezekano wa wanachama wetu kuingia katika mkumbo wa tuhuma zisizowahusu. Chama cha Wanasheria Tanganyika ni Mwanachama wa Chama cha Wanasheria wa AfrikaMashariiki (EALS); Chama cha Wanasheria wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa(SADCLA); Chama cha Wanasheria Wanamajumui wa Afrika (PALU) na pia chama kinamakubaliano ya ushirikiano na wadau mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kwa sababu hiyo tunaamini kuwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kinao Uwezo mkubwa wa kutoamchango wake katika kulisaidia taifa katika maeneo mbalimbali yahusuyo haki jinai ya kimataifapia. VIlevile, katika kuongeza wigo wa upatikanaji haki jinai tunaiomba Serikali yetu ilifanyie


kazi ombi letu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kurejesha tamko lake la kuruhusu raia waTanzania kufungua mashauri katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Umma chini yaIbara ya 34(6) ya Itifaki inayoanzisha Mahakama hiyo.

 

Mhe. mgeni rasmi,

IV Kuimarisha Uhusianio kati ya Mahakama na Chama cha Wanasheria Tanganyika

Kwa kuhitimisha, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika tunaamini kuwa ushirikiano nauhusiano mzuri kati ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika na Mahakama ni wa kudumu nausioepukika. Kuna wakati wanachama wetu wanaingia katika mgogoro na sheria. Wakati mwingine wanachama wetu wanashtakiwa katika Kamati za kusimamia maadili ya mawakili.Wakati mwingine kumekuwa na maamuzi ambayo mawakili watuhumiwa wanaona kwamba hawakutendewa haki. Chama chetu kimeendelea kuhimiza wanachama na wadau wake waendelee kuheshimu maamuzi yote ya Mahakama kwani huo ni msingi imara wa utawala washeria. Hata hivyo, bado tunaiomba Mahakama iratibu wadau wa haki kikiwemo Chama cha Wanasheria wa Tanganyika ili kufanya maboresho ya sheria na kanuni zinazosimamia nidhamuza Mawakili kwa lengo la kuweka misingi bora zaidi ya usimamiaji wa haki. Vilevile tunaiomba Mahakama itenge ofisi ambayo itakuwa ni Ofisi rasmi ya Kamati ya Mawakili (Advocates Committee) ili kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu uwasilishaji wa nyaraka na ufuatiliaji wa maamuzi au nyaraka zinazotoka katika Kamati hiyo. Hatua zote hizi zitasaidia pia utoaji wa hakipale ambapo Wakili anatuhumiwa aweze kutendewa haki pasipo shaka, pasipo kuonewa na bilakupendelewa. Ni ombi letu kwamba, tutakapokuwa tunazungumzia upatikanaji wa hakituhakikishe kuwa pia haki inapatikana hata kwa upande wa Mawakili pale ambapo wanakuwa wakituhumiwa. Naomba uniruhusu nimnukuu Mheshimiwa Jaji Mkuu Msaafu


Mhe. Barnabas Albert Samatta katika kitabu chake cha Utawala Bora: vita dhidi ya udhalimu, rushwa na elimu duni (ukurasa wa 3) ambapo anasema kwamba Katika Maisha ya ustaarabu,sheria inaelea katika Bahari ya maadili. Pia anasema (katika ukurasa wa 39) kwamba: Ni sahihizaidi kuwa utawala wa sheria utawale kuliko mtu yeyote. Utawala wa sheria unamaanisha kuwakila mtu anawajibika kwa sheria, wakiwemo watu ambao ni watunga sheria, watekelezaji wa sheria na majaji. Wito wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika ni kwamba katika kusimamia maadili ya Mawakili, Mahakimu, Majaji na Waendesha Mashtaka iko haja ya kupitia upya nakisha kuboresha misingi ya utawala wa sheria katika eneo hilo ili kuhakikisha kwamba usimamizi wamaadili yao unazingatia kwa dhati misingi pamoja na kanuni za haki ya asili (Principles of NaturalJustice). Tunafahamu sote kuwa kanuni hizo zinakataza mlalamikaji kuwa ni hakimu kenye kesiinayomhusu, na pia inahimiza kuzipa fursa pande zote mbili kusikilizwa kikamilifu. Misingi hii litasaidia kuondoa mivutano na misuguano kati ya Mawakili na wadau wengine katika sekta ya haki.

 

Mwisho kabisa, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, kinafahamu na kinaipongeza sana Mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika matumizi yaTeknolojia. Tunaiomba Mahakama, kwa kuzingatia kwamba Mawakili ni Maofisa wa Mahakama, na Mawakili ni watumizi wakuu wa huduma za Mahakama, changamoto za kimfumo ziwe zikitatuliwa kwa wepesi na pia matumizi ya teknolojia yatakuwa na tija zaidi ikiwa uboreshaji waTeknolojia ungefanyika pia katika Chama cha Wanasheria wa Tanganyika na kuhakikisha kuwaMawakili wote wanaouwezo, nyenzo na teknoilojia hii itakayoboresha sana upatikanaji wa haki.


Mheshimiwa Mgeni Rasmi

Kwa kweli siku ya leo ni siku muhimu sana kwa wadau wa sheria, na tumekusanyika hapa nakwingine kote nchini katika mikoa yote ya Tanzania Bara kuadhimisha siku hii ambapomaonyesho yalianza tarehe 27/01/2024 yakizinduliwa kwa matembezi na kufuatiwa nashughuli za kutoa elimu kwa umma pamoja na shughuli nyingine za kuelimisha jamii. Hivyo tunaamini kwamba, maoni na mapendekezo yaliyotolewa na wadau katika siku hii muhimu yatatiliwa maanani na kufanyiwa kazi ili kuleta tija ya ushiriki wa wadau katika siku hiimuhimu, na kwa manufaa ya Watanzania na Taifa letu zuri la Tanzania kwa ujumla. Siku hiiinaweka alama chanya kuwa mwaka wa kazi za Mahakama unaanza rasmi, hivyo tunawatakia utendaji mwema wa shughuli zote huku nasi tukianza maandalizi ya kusherehekea miaka Sabiniya TLS.

 

Kama kauli mbiu ilivyo, kuhusu UMUHIMU WA DHANA YA HAKI KWA USTAWI WA TAIFA,naomba nimalize kwa kunukuu Kitabu cha Nabii Suleiman cha Mithali katika Sura ya 14:34kwamba: ’Haki huinua taifa; bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.’’‘Justice exalteth a nation; but sin is a reproach to any people.’

 


NAOMBA KUWASILISHA ASANTENI KWA KUNISIKILIZA. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Comments

Popular posts from this blog