MAFUNZO YA KUJENGEA UWEZO MAOFISA ZAIDI YA 40 WA JESHI LA POLISI NA MAGEREZA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA VIZUIZINI
Huduma ya Msaada wa Kisheria Yafika Halmashauri ya Rorya, Mara: Wananchi wa Kata ya Bukura, Kijiji cha Bubombi na Kirongwe Wapata Mafunzo Kuhusu Haki na Sheria Muhimu Katika muendelezo wa utekelezaji wa utoaji huduma ya msaada wa kisheria, timu ya afisa maendeleo ya jamii kutoka Halmashauri ya Rorya, Mara, ilitua katika kata ya Bukura, kijiji cha Bubombi na Kirongwe kwa lengo la kuwafikia wananchi na kuwajulisha juu ya uwepo wa dawati la msaada wa kisheria ndani ya halmashauri yao. Wananchi walipata fursa ya kujuzwa kuhusu namna dawati hili linavyofanya kazi na umuhimu wake katika utoaji wa haki. Wakati wa ziara hiyo, mada mbalimbali zilijadiliwa kwa kina, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi, Sheria ya Ndoa, Mirathi na Wosia, Ukatali wa Kijinsia, Utatuzi wa Migogoro, na Haki za Watoto. Huduma hii ni sehemu ya juhudi endelevu za kuhakikisha wananchi wanapata taarifa muhimu na msaada wa kisheria ili kutatua changamoto zinazowakabili katika jamii zao.



Comments
Post a Comment