NAIBU WAZIRI SAGINI ASIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KATIKA BANDA LA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA, WANANCHI WATOA SHUKRANI KWA RAIS SAMIA- SABASABA, DSM 

Mhe. Jumanne Abdallah Sagini (Naibu Waziri wa Katiba na Sheria) leo tarehe 5 Julai, 2024, ametembelea banda la Wizara hiyo na kujionea utoaji huduma katika Kampeni ya Msada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign)


Akiwa katika banda hilo lililopo katika viwanja vya maonesho vya sababa vilivyopo Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam, Naibu Waziri Sagini amezungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo na kusikiliza na kutoa msaada wa utatuzi wa changamoto zao.

Nao wananchi wamemthibitishia kupatiwa huduma hiyo kwa kusikilizwa kwa weredi mkubwa na kwa haraka ambapo wametoa shukrani zao za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha kampeni hii.

Pia, Naibu Waziri Sagini ametoa wito kwa watanzania wote kuendelea kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya sabasaba kwenye banda hilo kwakuwa kampeni hiyo pia imekuwa ikitoa ushahuri katika changamoto mbalimbali za masuala ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuyamaliza kabisa.

Aidha, Naibu Waziri Sagini akizungumza na wanahabari juu ya Mpango wa Wizara katika kuwasaidia wanachi , amesema;


" Lengo la Wizara ni kuendelea kutumia fursa hii na mtizamo wa Wizara haswa kwa Waziri wetu Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, katika kuhakikisha dhamira ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ya kila mwananchi kupata haki inatekelezwa kwa vitendo na kuwafikia wananchi wengi kupitia kampeni hii na hadi sasa imefikia mikoa 7 na itaandaa wataalamu ngazi ya mikoa ambao watashuka hadi ngazi za wilaya zote nchini na kuhakikisha hadi kufikia mwakani tuwe tumefikia mikoa yote. "

Vilevile, Naibu Waziri Sagini amebainisha kuwa , " Maonesho ya sabasaba yanawafikia watu wengi ndio maana hata leo kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 9 alasiri tayari tumehudumia watu zaidi ya 40 "

Lengo la kampeni hii ni kushughulikia migogoro ya ardhi, kutoa msaada wa kisheria katika changamoto au tatizo lolote na utekelezaji wa sera za kisheria ambapo bando hilo la huduma litaendelea kutoa huduma hadi ifikapo tarehe 13 Julai, 2024.

#MSLAC

Comments

Popular posts from this blog