WAKAZI WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA
Wakazi wa Mkoa wa Arusha wamejitokeza kwa wingi kushiriki katika kampeni ya msaada wa kisheria iliyoanzishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kampeni ambayo ilizinduliwa rasmi leo mkoani humo. Kampeni hii inalenga kuwawezesha wananchi kwa kuwapa elimu kuhusu haki zao za kisheria na kusaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili. Katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Paul Christian Makonda, waliongoza shughuli za utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi. Kliniki za kisheria ziliwekwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa, ambapo wananchi walihudhuria kwa wingi na kupata fursa ya kushauriana na wataalamu wa sheria kuhusu changamoto zao, zikiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, masuala ya kifamilia, na haki za kijinsia. Akizungumza na wananchi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Jumanne Sagini, aliwahimiza wakazi wa Arusha kutumia fursa hii muhimu...






Msaada wa kisheria ni bure kwa kila Mkoa , kwa kila Halmashauri, kila kata, kila kijiji, Msaada wa kisheria ni haki, usawa, Amani na maendeleo
ReplyDelete#SisiniTanzania
#MSLAC
#matokeochanya
#sisindiowajenziwaTanzaniayetu
#nchiyangukwanza
#naipendanchiyangu
#SSH
#kaziiendelee
Huduma ya msaada wa Kisheria wa mama Samia ni Daraja la Elimu na msaada wa Kisheria Kwa Wananchi Wote hasa wenye kipato duni ambao wanashindwa kumudu gharama za mawakili.
ReplyDelete#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
Mama kawafikia pia wasio weza kukidhi haja ya kulipa mwanasheria Kusimamia kesi zao, kupitia MSLAC ni bure
ReplyDeleteUsiruhusu kukosa uelewa wa sheria kukunyima haki zako. Kampeni ya Msaada wa Kisheria (MSLAC) inakuletea msaada wa kisheria na elimu bila malipo kwa wote. 🇹🇿
ReplyDelete#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya