MSLAC KUINUA ELIMU YA UTAMBUZI HAKI, USAWA, AMANI NA MAENDELEO KWA WATANZANIA WALIO NA UHITAJI NA WASIOJIWEZA.
Msaada wa kisheria ni njia ya kuhakikisha kuwa watu wote, hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kifedha, wanapata fursa ya kutetea haki zao mahakamani au kupitia njia za nje ya mahakama kama usuluhishi na upatanishi. Kupitia msaada wa kisheria:
Wananchi wanaelimishwa kuhusu haki zao za kisheria, kama haki ya ardhi, mirathi, ajira, ndoa, na kuzuia ukatili wa kijinsia.
Wanasaidiwa kufungua na kufuatilia kesi zao mahakamani au kuandika nyaraka za kisheria, kama wosia au mikataba.
Haki inapatikana kwa wote, si kwa wale wenye uwezo wa kifedha pekee.
Msaada wa kisheria huchangia amani kwa kupunguza migogoro inayotokana na ukosefu wa maarifa ya kisheria na ukosefu wa upatikanaji wa haki.
- Njia mbadala za utatuzi wa migogoro, kama upatanishi na usuluhishi, husaidia kupunguza uhasama kati ya pande zinazohusika.
- Wananchi wanaopewa msaada wa kisheria wanakuwa na imani na mfumo wa haki, hivyo kuepuka kujichukulia sheria mikononi mwao.
Msaada wa kisheria hutoa nafasi sawa kwa watu wote bila kujali jinsia, hali ya kiuchumi, au jamii wanayotoka.
- Hupunguza tofauti kati ya matajiri na maskini katika kupata haki.
- Hukuza usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wanapewa msaada wa kutetea haki zao dhidi ya ukatili wa kijinsia au unyanyasaji.
Msaada wa kisheria ni nyenzo muhimu ya maendeleo kwa sababu unasaidia
- Kuimarisha ustawi wa jamii kwa kuhakikisha haki za kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni zinalindwa.
- Kupunguza umasikini kwa kutoa mwongozo kuhusu masuala ya ajira, mikataba ya kazi, na fidia kwa wafanyakazi.
Kujenga jamii yenye maarifa ya kisheria, hivyo kuongeza uwajibikaji na ustawi wa kijamii.
Elimu ya sheria inawawezesha wananchi kuelewa haki na wajibu wao, hivyo kusaidia kutatua migogoro kwa njia za amani na kuimarisha usawa wa kijamii🇹🇿#MSLAC #Katibanasheria #SSH #CCM #KaziIendelee #Nchiyangukwanza #SisiniTanzania #matokeochanya
ReplyDeleteHakika MSLAC ni mkombozi wa haki
ReplyDeletepongezi kwa serikali chini ya uongozi wa dr Samia Suluhu Hassan kwa kuanziSha dawati la msaada wa kisheria ambalo linatoa huduma pamoja na elimu ya msaada w kisheria kwa wananchi ili kuwajengea uelewa katika kutambua na kuzifikia haki zao #SisiNiTanzania #HayaNdioMatokeoChanyA #mslac #SSH #SioNdotoTena #SisiNdioWajenziWaTanzaniaYetu #kaziiendelee
ReplyDeleteElimu ya msaada wa kisheria ni mkombozi kwa migogoro iliyopo katika jamii nyingi za Tanzania. #sisinitanzania #hayandiomatokeochanya #mslac #katibanasheria #machalatandawili
ReplyDeleteMama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC) ina lenga kukuza Usawa na Haki za Binadamu
ReplyDeleteKwa kuangazia masuala ya usawa wa kijinsia, haki za watoto, na vikundi vilivyo hatarini kama watu wenye ulemavu.
Kutoa msaada wa kisheria na kijamii kwa watu wanaokandamizwa au kunyimwa haki zao.