MSLAC - KATATUA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI KILOSA.


Dawati la msaada wa kisheria wilayani Kilosa limefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima katika vijiji vya Nyali na Zombo Lumbo. Katika mazungumzo ya usuluhishi, ilibainika kuwa upande wa wafugaji ulishindwa kuthibitisha umiliki halali wa maeneo hayo.  

Vijiji hivyo vipo chini ya mpango wa matumizi bora ya ardhi, ambao haujatenga eneo maalum kwa ajili ya shughuli za ufugaji. Kutokana na hali hiyo, ilithibitishwa kuwa wafugaji waliingia kwenye maeneo ya wakulima kinyume na sheria. Baada ya kupokea ushauri wa kisheria kuhusu umiliki wa ardhi na mpango wa matumizi, wafugaji waliridhia kuondoa mifugo yao ndani ya siku 14.  


MSLAC limefanikiwa kumaliza mgogoro binafsi kati ya Diwani wa kata ya Zombo na wafugaji waliokuwa wakimlalamikia kwa madai ya unyanyasaji na upendeleo kwa wakulima. Pande zote zilifikia maridhiano, na hatua hiyo imeleta utulivu katika eneo hilo. 

Comments

  1. Elimu ya msaada wa Kisheria Kwa haki, Usawa, Amani na maendeleo
    #SisiNiTanzania
    #HayaNdioMatokeoChanya
    #Katiba_sheria
    #MSLAC
    #DrSSH
    #Kaziiendelee

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog