MSLAC YAZINDULIWA KWA KISHINDO DAR ES SALAAM – VIONGOZI WAKUU WA TAIFA, WANASHERIA NA WASANII WAJITOKEZA KWA WINGI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA
Katika tukio la kihistoria lililofanyika tarehe 16 Juni 2025, maelfu ya wananchi walijitokeza katika viwanja vya Maturubai, Mbagala – Dar es Salaam, kushuhudia uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (MSLAC). Hafla hiyo ya kipekee iliongozwa na Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).
MSLAC ni kampeni inayolenga kuwafikia wananchi wa kawaida na kuwapatia elimu ya kisheria, msaada wa kisheria bure, haki za msingi, na kujenga jamii yenye uelewa wa sheria, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya haki jumuishi inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Comments
Post a Comment