KLINIKI YA MSAADA WA KISHERIA MOROGORO: WANANCHI WAPATIWA HUDUMA ZA HAKI KARIBU NA MAKAZI YAO.
Katika Stendi ya Zamani ya Mabasi, Manispaa ya Morogoro Mjini, wananchi wanaendelea kunufaika na huduma za msaada wa kisheria zinazotolewa kupitia banda la Wizara ya Katiba na Sheria. Kupitia Kliniki ya Msaada wa Kisheria, mwananchi amekabidhiwa hati ya kiapo kwa ajili ya kuwasilishwa mahakamani ili kumuwezesha kuwa msimamizi wa mirathi. Huduma hii ni sehemu ya jitihada za serikali kusogeza haki karibu na wananchi, kutoa elimu ya kisheria, na kusaidia jamii kutatua changamoto zao za kisheria kwa urahisi na ufanisi.