Waziri Juma Homera Akagua Utendaji wa Taasisi za Katiba na Sheria Morogoro


Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Juma Homera, amefanya kikao maalum na watendaji walio chini ya Wizara hiyo katika Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuakisi na kutathmini utendaji wa Wizara na taasisi zake katika mkoa huo. Kikao hicho kimewakutanisha viongozi na watumishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (OSG), Mahakama ya Tanzania pamoja na Wakala wa Ufilisi na Usaili (RITA).




Katika mkutano huo, Mhe. Homera alisikiliza taarifa za utekelezaji wa majukumu, changamoto zinazowakabili watendaji pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika utoaji wa huduma za haki na kisheria kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro. Waziri alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ushirikiano wa taasisi na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha haki, usawa na utawala wa sheria.












Mhe. Homera aliwahimiza watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi, akibainisha kuwa Wizara itaendelea kutoa ushirikiano na maboresho yatakayowezesha taasisi zake kutekeleza majukumu kwa ufanisi zaidi kwa manufaa ya wananchi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Comments

Popular posts from this blog

MSLAC YAZIDI KUIMARISHA UPATIKANAJI WA HAKI KWA WANANCHI NCHINI TANZANIA

VIONGOZI SONGEA NA MADABA KUPATIWA ELIMU YA UTATUZI WA MIGOGORO SEKTA YA SHERIA